Mkurugenzi Mtendaji na Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mwl. Zainabu J. Makwinya, amewahamasisha wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Orodha ya Wapiga Kura ili kuwa na sifa wa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27,2024.
Mwl.Makwinya ametoa rai hiyo, akimwakilisha, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Amir Mkalipa kama Mgeni kwenye Ligi ya Mpira wa Miguu iliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Uwiro Mhe. Dauson Urio, Ligi iliyopewa jina la DIWANI CUP.
Hata hivyo, Mwl. Makwinya amepata fursa kutoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Uwiro kuhusu uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa kwa ngazi ya vijiji na vitongoji pamoja na kueleza sifa za mpiga kura Kugombea kwenye Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa.
"Katika halmashauri yetu, uchaguzi utahusisha Wenyeviti wa Vijiji na wenyeviti wa vitongoji na kila mwananchi anatakiw akutumia haki yake ya kikatiba ya kupiga kura kwa kujiandiskisha kwenye eneo analoishi kwenye vituo vilivyoanishwz kuanzia tarehe 11- 20 Oktoba 2024, kila mkazi mwenye umri wa kuanzia miaka 18 anapaswa kujiandikisha na hatimaye kupiga kura ifikapoNovemba 27,2024"Amesisitiza Mwl.Makwinya
Licha ya Mkurugenzi huyo kuwataka wananchi kuchagua viongozi wenye sifa wenye uwezo wa kusukuma gurudumu la maendeleo kwenye vijij8 na vitongoji vyao, amewahamsisha kugombea nafasi hizo ili kuaota kiongozi bora.
Naye, Afisa Uchaguzi halmashauri hiyo, Edward Bujune, amegawa vipeperushi kwa wananchi vyenye maelezo yanayohusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vikionyesha sifa za wagombea na wapiga kura pamoja na tarehe za kujiandikisha na tarehe ya Uchaguzi.
Hata hivyo, Katika uhamasishaji huo uliofanyika katika Kata ya Uwiro wananchi wamepatiwa elimu ya utofauti wa kujiandikisha kwenye daftari la Wakazi na Vitambulisho vya Kura vitakavyotumika kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani 2025.
Timu zilizoshiriki katika mashindano ya fainali ya DIWANI CUP ni Timu ya Kivumbi na Timu ya Kimulimuli ambapo Timu ya Kimulimuli imeibuka Kidedea kwa mikwaju ya Penati goli 4-3 baada ya Mchuano mkali wa dakika 90 bila kufungana.
Mhe.Diwani Kata ya Uwiro Dauson Urio kwa niaba ya Wananchi wa Kata ya Uwiro yenye vijiji vitatu vya Kisimiri Juu, Kisimiri Chini na Uwiro ametoa shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji kwa kufika na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
"Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi".
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.