Naibu Waziri wa Afya nchini Tanzania Dkt. Godwin Mollel, akimfariji mmoja ya mgonjwa aliyefika kupata huduma za afya kwenye Kambi ya matibabu ya Bure inayotolewa na Madaktari Bingwa na Wabobezi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha Juni 29,2024, alipotembelea mabanda ya watoa huduma na kujionea hali ya utoaji na upatikanaji huduma kwa wagonjwa, ikiwa ni siku ya sita ya huduma hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutolewa kwa siku saba.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo, ameridhishwa na huduma hiyo njema kwa wagonjwa na kumponheza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda @baba_keagan kwa ubunifu huo, uliwezesha wananchi wenye changamoto za kifya kuhudumiwa na kurejesha matumaini ya maisha yao.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.