Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi nchini Tanzania Balozi Ndg. Dkt. Emmanuel Nchimbi akiingia kwenye Uwanja wa Standi ya Daladala Kilombero Jijini Arusha kwa ajili ya Mkutano wa Hadhara na wananchi wa Jiji hilo la Arusha Juni 03, 2024.
Katika Mkutano huo, Dkt. Nchimbi amezungumza na wananchi pamoja na kusikiliza na kutatua kero na changamoto zao huku akiwasisitiza wakazi wa Arusha kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuinga mkono Serikali ya awamu ya sita kwa kazi kubwa inyofanya ya kuwahudumia wananchi.
Katibu Mkuu huyo ameambatana na Katibu wa NEC- Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla Pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdalla Hamid wakiongozwa na mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.