Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, amewasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania, kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Kilimanjaro asubuhi ya leo Machi 6, 2024.
Makamu wa Rais, yuko mkoani Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa 21 wa Taasisi ya Fedha, unaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) Ukumbi wa Simba.
Mada Kuu katika Mkutano huo ni Kuimarisha Ustahimilivu wa Sekta ya Fedha Nyakati za Changamoto za Kiuchumi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.