Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpangoameiagiza Wizara ya Nishati kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya III mzunguko wa pili kuusimamia vema ili umeme huo uweze kusambaa maeneo ya vijijini na kupelekea wananchi kupata maendeleo.
Aidha ameahidi kuwasomesha bure watoto hao wawili kati ya watatu wa mama mjane Gladness Giloli hadi watakapomaliza kidato cha nne huku mtoto mwingine mdogo akiendelea na malezi ya mama yake
Dkt. Mpango alitoa agizo hilo katika kijiji cha Sale Wilayani Ngorongoro nyumbani kwa mjane huyo mwenye watoto watatu ambao ni Anita Ndinade (14) ,anayesoma darasa la saba,Farida Ndinade (12) anayesoma darasa la nne na Goodness Ndinade (3)
Dkt. Mpango aliagiza umeme huo uwafikie wananchi hao na wengine ili waweze kufanya shughuli mbalimbali za kimaendelo ikiwemo kujikwamua kiuchumi.
Pia alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella na uongozi wa wilaya ya Ngorongoro kwaumuzi wa kumuwashia umeme mjane huyo kupitia kifaa maalum cha Ometa chakupachika ukutani ndani ya nyuma pasipo kuwe
"Serikali ya Rais Samia Hassan Suluhu itakusomeshea watoto wako hawa wawili hadi kidato cha nne na usivunjike moyo kwani ujane sio mwisho wa maisha,tuzidi kumwomba mungu kwa maisha haya na usijali watoto watasoma bure"
Lakini pia wizara ya nishati kupitia mradi huu hakikisheni mnausimamia vema ili wananchi wa hali ya chini wapate huduma ya umeme na kujikwamua kiuchumi.
Awali ,Naibu Waziri wa Nishati,wakili Byabato alisema lengo la serikali ni kuwezesha kusambaza umeme vijijini kwa wananchi ikiwemo kuwafikia wananchi mbalimbali kwaajili ya maendeleo.
Alisema nyumba hiyo umeme wake unawaka kupitia kifaa maalum cha Ometa na kuongeza kuwa gharama ya kuunganisha umme vijijini ni sh,27000 na mahitaji halisi ya kuunganishiwa umeme ni sh,80,0000 lakini maeneo ya vijijini Rais Samia Hassan Suluhu aliamua kuchangia kwa wananchi gharama kubwa huku mwananchi wa kawaidia akichangia sh. 20000 tu.
Alisema katika eneo hili vijiji 42 vipo katika mradi huo wa umeme vijijini ambapo vijiji 21 vimeshawashiwa umeme na vijiji vingine 21 vipo mbioni kuwashiwa umeme huo wa REA hadi Disemba mwaka huu umeme utakuwa umewaka maeneo yote
Alisema mradi huo wa usambazaji umeme upo katika awamu nne awamu ya kwanza ni REA awamu ya I awamu ya II, awamu ya III na umeme jadidifu kwa kutumia Sola unakwenda katika vitongoji na ule unaopelekwa kwenye viwanda na maeneo mengine makubwa ambapo katika wilaya hiyo ya Ngorongoro jumla ya sh.bilioni 18.1 zimetengwa kwaajili ya kusambaza umeme vijijini na maeneo mengine wilayani hapo ambapo katika kijiji cha Sale jumla ya sh. bilioni 1.4 zimeletwa kwaajili ya kusambaza umeme.
Awali Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Magunkune kata ya Sale ,Bashiri Sambode akisoma taarifa ya mradi huo wa Rea alisema umeme huo umewasaidia kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kuchaji simu,uuzaji wa vinywaji vya baridi,mafundi vyuma na nk.
Alisema umeme huo umerahisisha ufundishaji mashuleni kupitia projekta, kompyuta ikiwemo matibabu ya wagonjwa hospitalini
Huku mjane huyo,Gladness aliishukuru serikali kwa kujali wajane kwani yeye ni mjane mwenye watoto watatu na kuongeza kuwa umeme huo unamsaidia kujikwamua kiuchumi katika shughuli mbalimbali anazozifanya katika kujipatia kipato.
Alisema watoto wake walikuwa wanasoma kwa kutumia vijanga vya moto na kuelekea kuwa hatasahau siku moja watoto wake hao wawili wanaosoma walishindwa kufanya kazi za shule za jioni kwasababu ya kwakosekana kwa umeme.
"Nashukuru Mungu kwa umeme huu kwani kunasiku moja watoto wangu hawa wawili Farida na Anita walishindwa kufanya shughuli za masomo ya jioni sababu ya kukosekana kwa umeme lakini leo nashukuru umeme unawaka na watoto wangu wanasoma"
Wakati huo huo RC,Mongella alisema awali walifika eneo hilo na kuona changamoto mbalimbali anazopitia mama huyo ikiwemo kupambana katika shughuli za kujikwamua kiuchumi ili familia yake ipate mahitaji yao na kwasababu ya changamoto hizo alizonazo waliamua kumwekea kifaa hicho nyumbani hapo kwaajili ya kupata mwanga na kujikwamua kiuchumi
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.