Mkuu wa mkoa wa Arusha, mheshimiwa Idd Kimanta, amewaongoza wakazi wa mkoa wa Arusha na vitongoji vyake, kuuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, marehemu Richard Kwitega, shughuli iliyofanyika mapema leo, kwenye uwanja wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha.
Akitoa salamu za rambirambi mbele maelfu ya waombelezaji, wakiwemo wafanyakazi wa Idara na Taasisis malimbali za mkoa wa Arusha na mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Mkuu huyo wa mkoa, licha kuhuzunishwa sana, na kifo cha Bwana Kwitega amewataka waombolezaji hao kuyaishi matendo mema, aliyoyaishi marehemu Kwitega wakati wa uhai wake, kwa kudumisha upendo na ushirikiano mahala pa kazi.
Mheshimiwa Kimanta, amemuelezea Marehemu Kwitega, kuwa alikuwa ni mwenye mahusiana mazuri ya kikazi na kijamii katika eneo la kazi na kuongeza kuwa alikuwa ni kiungo na mhimili imara kati ya watumishi wa serikali, sekata binafsi, mashirika yasiyo ya kiserika pamoja na vyama vya siasa na daima alihakikisha shughuli na mipango yote ya serikali inatekelezeka ndani ya mkoa wa Arusha kwa mafanikio makubwa sana katika sekta zote.
Kama nii kipuri cha gari, Kwitega niliweza kumuita 'shokomzoba', alikuwa ni mhimili wa shughuli zote za mkoa wa Arusha, aliyefanyakazi bila kuchoka, bila ubaguzi, bila majungu na kumuheshimu mkubwa kwa mdogo. ninasema tanguli Richard, tangulia Richard, hii ni kazi ya Mungu, tunaamini na sisi tuko nyuma yako" Amesisitiza Mkuu wa mkoa kwa uchungu mkubwa.
Marehemu Richard Kwitwega, amefariki kwa ajali ya gari siku ya Jumatano tarehe 03.02.2021, eneo la Mdorii mkoani Manyara, akiwa njiani kuelekea mkoani Dodoma na mwili wake unasafirishwa leo kuelekea mkaoni Mwanza wilaya ya Sengerema kwa mazishi yatakayofanyika siku ya Jumamosi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.