*UGENI*
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro(MB), amefika kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, na kusaini kitabu cha wageni, na baadaye kufanya mazungumzo mafupi na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella, leo tarehe 18 Desemba, 2023.
Akiwa mkoani Arusha, pamoja na shughuli za kikazi, Mhe. Ndumbaro atafanya ziara ya kutembelea kata ya Olmot, eneo linalotarajiwa kujengwa uwanja wa mpira wa miguu, utakaotumika kwenye mashindano ya AFCON mwaka 2027.
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.