Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia amesema Serikali ya awamu ya sita imeshatoka fedha zote za lishe kwa Mkoa wa Arusha.
Ameyasema hayo alipokuwa akifunga kikao cha kamati ya lishe cha Mkoa, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
"Kilichobaki kwa sasa ni jukumu letu la kutekeleza wajibu wetu kwa kuhakikisha viashiria vyote vya afya katika lishe vinatekelezwa katika ngazi za Halmashauri".
Aidha, Dkt.Kihamia amewataka wadau wa lishe waendelee kutekeleza wajibu wao kwa nafasi yao na Serikali itafanya kwa nafasi yake ili kuinua zaidi swala zima la lishe katika Mkoa.
Nae,Afisa lishe Mkoa wa Arusha Bi. Rose Mauya amesema kwa ngazi ya Mkoa wameshajipanga kufanya ufuatiliaji wa karibu zaidi katika halmashauri zote ili kuhakikisha wanatoa fedha za lishe kwa watoto chini ya miaka 5.
Mkoa amewawekea Halmashauri utaratibu wa kuzipima kwa kutumia kadi maalumu zenye viashiria vyote vya lishe, haya yamesemwa na Afisa ustawi wa Jamii bwana Denis Mgiye katika kikao hicho.
Vile vile, Dkt. Frida Mokiti kutoka kanisa katoriki ameishauri Serikali kuongeza kasi ya usambazaji wa dawa za kuongeza damu katika vituo binafsi ili kuwezesha huduma hiyo kuwafikia watu wengi zaidi.
Mwakilishi kutoka taasisi inayojishughulisha na wanawake na watoto( center for women and children development) Bi. Hindi mbwego. amesema ni wakati sasa umefikia kwa watoto wa shule kupatiwa chakula wakiwa mashuleni ili waweze kuzingatia masomo yao.
Kamati ya lishe ya Mkoa imekutana na kufanya tathimini ya hali ya lishe kwa Mkoa wa Arusha na kuweka mikakatika ya kuondoa udumavu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.