Fedha za mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) zinalenga kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu bwana Said Mabiye alipokuwa akikagua mradi wa kivuko katika halmashauri ya Arusha.
Aidha,Imetaka Halmashauri hiyo kuhakikisha kivuko hicho kinamalizika kabla ya Juni 30, 2022 ili kuwarahisishia wananchi uvukaji hasa katika kipindi cha mvua.
Amesema changamoto kubwa waliyokuwa wanaipata wananchi wa kata ya Moivo ni uvukaji kutoka upande mmoja kwenda mwingine katika kipindi cha mvua.
Bwana Mabiye amesema Mkoa utahakikisha miradi yote TASAF inakamilika kwa wakati na kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.
Diwani wa Kata ya Moivo Selina Mollel amesema kivuko hicho kitatua changamoto kubwa kwa wananchi kwani walikuwa wanashindwa kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine na kukata mawasiliano hads nyakati za mvua.
Amesema kupitia mradi wa TASAF waliweza kuibua mradi huo na ukafanikiwa kupatiwa fedha kiasi cha Milioni 33.3 hadi kivuko kukamilika.
Zoezi la ukaguzi wa miradi ya TASAF unaendelea kufanywa na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kujionea hali ya miradi inavyoendelea katika halmashauri zote.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.