Waandishi wa habari wa Redio jamii wametakiwa kutumia taaluma yao katika kujenga nchi ambayo imejengwa kwa muda mrefu ikiwa na umoja, amani na mshikamano.
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Kimanta alipokuwa akifungua kikao kwa vyombo ya habari vya redio za kijamii katika siku ya upatikanaji wa habari.
Amewataka wakazingatie maadili ya taaluma zao katika utoaji wa habari zao ili jamii iweze kupata taarifa za kuwaelimisha na kuijenga jamii husika katika nyanja mbalimbali.
Aidha, amewashauri katika utoaji wa taarifa zao wajitaidi kuonesha jinsi nchi yetu inavyojenga mahusiano na nchi nyingine.
Kimanta amesema, waandishi wa habari wakifanya kazi zao kwa weredi itawasaidia kuwajengea heshima wao kama wao na vyombo vyao vya habari.
Amesisitiza kwa waandishi wa habari kuzingatia usalama wao kwanza wakati wanafanya kazi zao za kiuwandishi wa habari.
Nae, Mkurugenzi wa taasis ya Maendeleo ya habari Tanzania (TADIO) bwana Prosper Kwigize amesema, kila mwaka taasis yake inasimamia siku ya upatikanaji wa habari dunia kila ifikapo Septemba 28 kwa lengo la kuhakikisha vyombo vya habari vinapata nafasi ya kupaza sauti kwa kueleza mambo mbalimbali yanayowahusu.
Hata hivyo bwana Kwigize, amesema vyomo vya habari hususani redio za kijamii zinatakiwa kufuata maadili ya uwandishi wa habari, ili kazi hiyo iweze kunufaisha jamii zetu za Kitanzania.
Amesema changamoto kubwa wanazokumbana nazo waandishi wa redio jamii ni waandishi wa habari wengi kutokuwa na ajira rasmi katika vyombo vyao na hivyo kuwafanya kutokuwa na uhakika wa ajira zao.
Kikao cha kuadhimisha siku ya upatikanaji habari duniani kimewakutanisha wanachama wa taasis hiyo ya TADIO ambao ni radio za jamii na kuweza kujadili muktaza na mwelekeo wa vyombo hivyo vya habari hususani kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.