Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha kuendelea kusimamia miradi mingine ya maendeleo.
Ameyasema hayo alipokuwa akikabidhiwa madarasa 9 yalikamilika kutoka kwa Halmashauri ya Arusha.
"Tusijisahau kuwa kuna miradi mingine ya maendeleo kama vile Maji, Barabara na Afya yote hii inatakiwa kuendelea pia".
Miradi ya kusimamia ili ikamilike ni mingi sana tusiweke nguvu nyingi kwenye hii miradi ya UVIKO 19 peke yake lazima hata hiyo miradi mingine nayo iendelee vile vile.
Halmashauri ya Arusha ilipatiwa fedha Bilioni 2 za mpango wa maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 100 na takribani madarasa 76 yamekamilika na 24 yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.