Watumishi wa Mkoa wa Arusha wahimizwa kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia maadili ya utumishi watu ili kuleta maendeleo katika Mkoa, kwani hakuna haki bila wajibu.
Yamesemwa hayo na Katibu Tawala wa Mkoa bwana Richard Kwitega alipokuwa akifungua kikao cha baraza la watumishi wa Mkoa wa Arusha kwa lengo la kujadili na kupitisha bajeti kwa mwaka 2019/2020.
Kwitega amesema,Serikali ya awamu ya tano imejikita zaidi katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi hivyo watumishi wa umma wanapaswa kuisimamia kwa umakini.
Miradi yote ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia bajeti za Serikali zinazopitishwa kila mwaka na kwa mwaka wa fedha 2019/2020 baraza la watumishi mkoa wa Arusha imepitisha bajeti ya kiasi cha shilingi Bilioni 7 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya ofisi na shughuli mbalimbali ya maendeleo.
Nae afisa kazi kutoka ofisi ya Kamishina wa kazi Mkoa wa Arusha bwana Emmanuel Mwita amesema, baraza hili linamanufa sana kwa watumishi wa umma kwani inawasaidia kufahamu mambo mbalimbali katika Mkoa.
Pia, watumishi wanapata nafasi ya kufahamu bajeti nzima na matumizi yake katika Mkoa na kama kutakuwa na mapungufu baraza hili linawapa nafasi ya kupendekeza na kushauri.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Arusha bwana Magero Samweli amesema,baraza hili linasaidia kuweka mazingira ya wazi kati ya mwajiri na mwajiriwa ambapo mwajiriwa anapata nafasi ya kufahamu kile kinachotekelezwa na Serikali yao.
Pia, amesema baraza hili nila muhimu sana kwa watumishi kwani inaondoa sitofahamu kwa watumishi kwani kila kitu kinakuwa wazi na watafahamu namna changamoto zoa zitakavyotatuliwa na kuongeza ufanisi kwao.
Baraza la watumishi Mkoa wa Arusha limejumuisha wakuu wa idara, vitengo na baadhi ya watumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Makatibu Tawala wa Wilaya na baadhi ya Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.