Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amezielekeza halmashauri zote Tanzania Bara kupanda miti pembezoni mwa barabara ili kuipendezesha miji na kuhifadhi mazingira.
Dkt. Jafo ametoa maelekezo hayo wakati akizindua ‘Mradi wa Twiga wa Kijani’ unaohusisha zoezi la upandaji wa miti katika shule za 60 za mikoa sita ya Tanzania, leo Machi 28, 2024 katika viwanja vya Shule ya Msingi Jeshini, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Amelipongeza Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kuliwezesha Shirika lisilo kiserikali la WBM kwa kuandaa mradi huo na zoezi la upandaji wa miti aliloliongoza akisema kuwa litasaidia kuwajengea wanafunzi ari ya kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira.
Amesema kuwa Tanzania imekuwa ikitembelewa na wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani hususan baada ya kuzalishwa kwa filamu ya ‘Royal Tour‘ na Serikali kununua ndege nyingi zaidi hivyo ni muhimu tukatengeneza madhari ya kuvutia pembezoni mwa barabara kwa kupanda miti.
Waziri Dkt. Jafo ameyataka majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Tanga, Mbeya, Arusha na Dodoma kuwa ya mfano wa kuigwa katika kutekeleza maelekezo ya kupandwa miti pembezoni mwa barabara.
Halikadhalika, amewaelekeza wakurugenzi wa halmashauri za manispaa kusimamia zoezi la usafi katika maeneo yao kwa kuwa na wakandarasi wa usafi wenye vifaa bora.
“Haipendezi hata kidogo unafika katika jiji fulani au manispaa fulani uchafu umetapakaa katika mitaro mvua ikinyesha mitaro inaziba na wakati mwingine malori ya yameegeshwa wakandarasi hawajatoa taka, nielekeze tena mtekeleze maelekezo hayo, imani yetu halmashauri zetu zitakuwa safi,“ amesisamesis
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.