Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amezitaka Halmashauri za Mkoa wa Arusha kuwa na mipango inayotekelezeka.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Longido,katika ziara yake ya kujitambulisha na kukagua miradi ya maendeleo.
"Shida ya mipango mingi ya halmashauri ipo kwenye makablasha tu haina dira wala haijawai kutekelezeka.
Ifika wakati sasa mipango mnayoweka mkaifanyie kazi ili ikalete tija kwa wananchi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Mipango hiyo ili itekelezeke ni lazima watumishi mjishushe kwa wananchi na inabidi utalaamu wenu kuweka pembeni kidogo na kwenda na hali halisi ya wananchi mfanye hivyo.
Nae, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Mhe. Oitesoi Laizer amesema balaza la madiwa na watumishi wanafanya kazi ushirikiano mzuri pamoja na ofisi ya Wilaya.
RC Mongella anaendelea na ziara yake ya kujitambulisha na kukagua miradi ambayo itapitia na Mwenge maalumu wa Uhuru katika Wilaya zote 6 za Mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.