Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Justine Nyamoga, imetoa rai kwa Halmashauri mbalimbali nchini kutumia mapato ya ndani katika kutekeleza miradi mbalimbali ya afya, elimu na miundombinu ili kufanikisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati Mhe. Nyamoga wakati wa ziara ya ukaguzi wa Miradi ya afya na miundombinu ya Barabara katika Halmashauri ya Mji wa Njombe ambapo Kamati imetembelea kituo cha afya cha Kifanyi ambacho kimejengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa zaidi ya shilingi mil 600.
“Huu ni mfano wa halmashauri chache ambazo uwekezaji wao kwa mapato ya ndani unaenda kwenye vitu vinavyowagusa wananchi moja kwa moja” Nyamoga.
Amesema yafaa sasa halmashauri nyingine zijifunze namna sahihi ya kutumia mapato ya ndani ya halmashauri kwaajili ya kujenga huduma ambazo zitawagusa wananchi.
Pia akiwa katika majumuisho ya ziara hiyo Mhe. Nyamoga ameutaka uongozi wa Halmashauri zote mkoani Njombe kufanyia uchunguzi wa chazo cha udumavu kwa wztoto kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mikoa ili kuboresha na kutokomeza swala la udumavu Mkoani Njombe.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.