1. Kuipongeza Serikali ya Awamu ya sita kwa kuleta fedha nyingi za kutekelza miradi ya maendeleo kisteka kuliko kipindi chochote cha awamu zilizotangulia.
2. CCM inampongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Sekretarieti ya Mkoa pamoja na watalamu wa ngazi zotebkwa kusimamia kwa uadilifub na uaminifu shughuli za maendeleo ikiwemo miradi, ikiwa ni usimamizi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
3. Chama kinawapongeza wananchi wote wa Mkoa wa Arusha kwa kushiriki katika shughuli za ujenzi wa Taiga pamoja na kujitoa kwa hali na mali kushiriki katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya amendeleo katika maeneo yao.
4. Chama Kinaelekeza kupika maeneo yote ya Umma na kuyapatia Hati Miliki maeneo ya shule, zahanati, vituo vya afya na hospitali, ili kuepuka migogoro pamoja na wananchi kuvamia.
5. Shule zote za Bweni za Msingi na Sekondari zijengewe uzio kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na mali za shule.
6. Majengo yote ya shule yanayojengwa kwa sasa yawekwe mabati angavu kwa ajili ya kuzuia uharibifu unaotokana na popo na ambazo hazijajengwa ziwekewe taa za umeme ili kuwafukuza popo.
7. Shule zote ambazo hazina maeneo ya michezo, zitafutiwe utaratibu wa maeneo ya jirani kwa ajili ya kufanyia michezo.
8. Usomaji wa Taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo uoneshe hali ya uchangiaji wa wananchi wa maeneo husika pamoja na mapato ya serikali za kijiji.
9. Utekelezaji waMiradi yote inayofadhiliwa na KFW Benki ya Ujerumani, hairidhishi kwa kuwa utekelzaji wake unachukua muda mrefu na inatumia gharama kubwa ukilinganisha na gharama za kawaida za utekelezaji wamiradi ya Serikali.
10. Halmashauri zote zitenge fedha kupitia Mapato ya Ndani kununua vifaa vya maabara zote za masomo ya Sayansi kwenye shule zote za sekondari, ili maabara hizo zianze kufanya kazi.
11. Wazazi waelimishwe kuhusu uchangiaji wa chakula shuleni kwa kuwelekeza uchangiaji wa chakula shuleni sio hiari ni lazima kuwalipia watoto wao chakula kwa shule za kutwa.
12. Kufanyike msawazo wa watumishi wa afya na walimu kwa kuwa kuna baadhi ya maeneo kuna watumishi wengi na maeneo mengine hakuna hasa maeneo ya vijijini ili kurahisisha upatikananji wa huduma kwa wananchi wote.
13. Kuwe na ulinganifu wa mgawanyo wa fedha za miradi ya maendeleo kwa kata na vijiji vyote, kwa kuwa kuna baadhi ya kata zina miradi mingi na nyingine hazina miradi kabisa.
14. Halmashauri ziangalie upya suala la Mamlaka za Miji midogo kwenye maeneo yoo, kama zinaemdshwa kwa faida ama hasara na kama ni hasara waanze mchakato wa kuomba kuzifuta.
15. Kutokana na uharibifu mkubwa wa barabara zinazohudumiwa na TARURA, unaotokana na mvua, ipo haja ya kuangalia upya bajeti ya barabara ili wananchi wapte huduma wakati wote.
16. Kutokana na mmomomyoko wa maadili unaotokana na mwingiliano wa tamaduni za nchi za nje, wazazi, viongozi, jamii na kila wananchi kwa nafasi yake asimamie maadili ya Taifa letu
17. Majengo yote yanayojengwa yazingatie uwepo wa miundombinu ya watu wenye mahitaji maalumu hususan wenye ulemavu wa viungo
18. Shule zote zihamasishwe kupanda miti ya asili ili kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
19. Viongozi wa ngazi zote washiriki katika ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo kwenye maendeleo yao pamoja na usimamizi wa miradi ya Maendeleo.
20. Maafisa Kilimo na Ugani wasikae ofisini waemde kwa wakulika kutoa elimu kulima mazao yanayoendana na upungufu wa mvua pamoja ja mabadiliko ya tabia nchi ili kukabiliana na tatizo la chakula.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.