Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella ametoa mwelekeo wa maeneno ambayo wafanyabiashara wadogo(Machinga) hawatatakiwa kufanya biashara zao.
Ameyasema hayo alipokutana na kufanya kikao na viongozi wa wamachinga, wafanyabiashara na watumishi wa Jiji la Arusha, katika ukumbi wa Ofisi yake.
Ameyataja maeneo hayo kuwa ni maeneo ya ndani ya soko la Kilombero na soko kuu wamachinga hawatakiwi kuwepo ndani ili kuruhusu wateja kuingia na kutoka kwa urahisi.
Pia, amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. John Pima kuhakikisha soko la Muromboo linapangiliwa vizuri na machinga wasizibe Barabara.
Maeneo mengine ni nje ya maduka, kwenye kuta za Hospitali, vituo vya Afya na mashule yanatakiwa kuwa wazi, ili kuruhusu shughuli za maeneo hayo zifanyike kwa umakini zaidi.
Wamachinga wanatakiwa kupisha maeneo ya mitaro inayopitisha Maji na hifadhi zote za Barabara ili kiwawezesha waenda kwa miguuu kupita kwa urahisi.
RC Mongella amesema lazima Mkoa wa Arusha urudi katika hali yake ya zamani yenye mpangilio na kupendeza na ili hayo yote yawezekane ushirikiano ndio silaha muhimu na Jiji la Arusha ndio sura nzima ya Mkoa.
Akibainisha maeneo mapya yaliyopendekezwa kwa ajili ya masoko ya Machinga, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt John Pima, amesema maeneo ambayo baraza la madiwa Jiji la Arusha limeyapendekeza ni Soko la Samunge ambalo litapangiliwa vizuri.
Stendi ya daladala Kilombero, kiwanja namba 68 Kilombero, Machame luxury, Uwanja wa ulezi na eneo la Muromboo.
Dkt. Pima amesema maeneo hayo yote Serikali itaweka miundombinu kama vile Vyoo, Maji, Umeme na Barabara ili kuwawezesha wamachinga hao kufanya kazi kwa uhuru.
Nae, mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoa wa Arusha bwana Locken Masawe amesema wanaheshima maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu namna yakuwapanga wamachinga
Aidha, amesema wao kama wafanyabiashara wanapenda kuona Jiji la Arusha linapendeza hivyo wapo tayari kushirikiana na Serikali katika kulifanikisha zoezi hili.
Mwenyekiti wa wamachinga Jiji la Arusha bi. Amina Njoka amesema wao wamefurahishwa na namna Jiji lilivyoyapaendekeza maeneo ya masoko yao kwani hata wao ndio walikuwa wanayaoendekeza hayo.
Kikao hicho ni cha kwanza cha uzinduzi wa kwanza wa mpango wa kuboresha Jiji la Arusha hususani namna ya kuwapanga wamachinga katika Jiji la Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.