Kamishna msaidizi wa Hifadhi Eva Malya, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha amewakaribisha washiriki wote wa Land Rover Festival katika Hifadhi hiyo akiwaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha kwa muda wote watakaokuwa ndani ya Hifadhi hiyo iliyopo nje kidogo ya Jiji La Arusha.
Leo Oktoba 13, 2024, Magari zaidi ya 300 chapa Moja ya Land Rover yaliyokuwa yakishiriki kwenye Parade maalum ya Land Rovee Festival 2024 yanafanya Utalii ndani ya Hifadhi hiyo yenye Mlima wa pili kwa urefu nchini Tanzania na wa tano barani Afrika, ikiwa pia ndiyo hifadhi miongoni mwa hifadhi tano za Taifa zenye kuliingiza Taifa fedha nyingi zaidi.
Kuingia kwa magari haya takribani 300 kwa wakati Mmoja, kulingana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, kunafanya kuwekwa rekodi ya kuwa na magari mengi zaidi ya chapa moja ya Land Rover kuweza kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa kwa wakati Mmoja.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.