Watanzania wanaposherehekea miaka 60 Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wamehimizwa kutambua kuwa Muungano, una historia yake, inayopaswa kutunzwa na kuhifadhiwa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
Rai hiyo, imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, wakati wa maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano Mkoa wa Arusho, yaliyofanyika kwenye Hospitali ya Jiji la Arusha eneo la Njiro.
Mhe. Mtahengerwa ameweka wazi kuwa, kila mtanzania anapaswa kutambua kuwa, Muungano haukutokea hivihivi ulikuwa na historia ambayo inatakiwa kuhifadhiwa na kutunzwa kwa kusemwa kwa kutambua dhamira ya waasisi wetu Nyerere na Karume kutoka na mapenzi mema ya kuona sisi ni ndugu na tuendelee kuwa kitu kimoja.
Amesema kuwa, historia ya miaka mingi ya damu na ya kijamii, ikiwa ni tamaduni na mila zinazofanana na kuwasukuma waasisi wetu, kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar, wakimaanisha kiapo ambacho kitadumu bila kuvunjikq, hivyo ni vyema kuendelea kuwafundisha watoto masuala ya Muungano pamoja na kuwambusha tulikotoka, tulipo na tunapoelekea.
Ameyataja mambo muhimu yanayoimarisha Muungano ni pamoja na Uwepo wa Wizara ya Muungano inayoshughulikia kero mbalimbali za Muungano ili kuwa na usawa ambao unaimarisha Taifa la Tanzania kusonga mbele ambapo Waasisi walitaka kutokomeza umaskini na kuwa na mikakati ya kupunguza umasikini ikwemo TASAF ambayo imeendelea kuinua vipato vya wananchi wa pande zote na kuondoa umasikini nchini.
"Muungano umedumu kwa umahiri wa nchi yetu kwa kuhakikisha tunalinda amani ya Nchi yetu, tukiwa na ushahidi wa nchi ambazo ziliungana na kuvunjika zianishi kwenye migogoro mikubwa hivyo kila mtanzania anapaswa kuulinda umoja huu pamoja na kulinda amani ambayo ni tunu ya Taifa letu.
"Tusiache kutembelea msemo wa Umoja ni Nguvu na utengeno ni Udhaifu, tusikubali kwa namna yoyote kuligawa taifa la Tanzania, tuwe imara na kupaza sauti kwa watu wote wanaoleta chokochoko kwa lengo la kuvunja Muungano, mifano halisi tunayo kwa nchi za jirani, " Ameweka wazi Mtahengerwa
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.