Kuelekea Kilele cha siku ya wanawake duniani, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, ametambulisha sehemu mpya ya malazi na vyumba vya kulala wageni, vinavyopatikana kwenye bustani ya mzunguko wa Barabara ya Mnara wa saa 'Clock tower' ambapo watalii wa rika mbalimbali watakuwa wanapokelewa kwenye eneo hilo kabla ya kuelekea kwenye maeneo ya Utalii. Kwenye hotuba zake Mbalimbali Mhe. Makonda amekuwa akihamasisha umuhimu wa wananchi wa Arusha kubuni vivutio na bunifu mbalimbali katikati ya Jiji, vitakavyochochea na kuinua kiwango cha matumizi ya fedha kwa wageni na watalii wanaofika Mkoani hapa katika jitihada za kukuza uchumi wao binafsi na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.