Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda amewasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arusha na kupokelewa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Filician Mtahengerwa mapema leo Mei 30, 2024.
Mhe. Makondo yuko wilaya ya Arusha ikiwa ni siku ya sita na ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya Siku 6 za Moto Arusha, ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kuzungumza na wananchi Jiji la Arusha, mkuano utakaofanyika Kilombero kwenye Stendi ya Daladala.
Hata hivyo, Mhe.Makonda licha ya kusiani kitabu cha wageni amepokea taarifa ya wilaya hiyo, iliyowasilishwa na mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Mtahengerwa na kuzungumza na viongo na watendeaji wa wilaya na jiji la Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.