Mazingira wezeshi kwa watumishi wa umma ndio yatakuwa kichocheo cha wao kufanya kazi kwa bidii na kwa weredi wa hali ya juu, hali hii itasaidia pia kuboresha huduma zitolewazo.
Haya yamesemwa na katibu mkuu wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya alipokuwa akizindua idara ya huduma ya dharura na ajali katika hospitali ya mkoa ya Mt.Meru.
Dkt. Mpoki amesema, hatua zinazofanywa katika hospitali hiyo ni kubwa na nzuri sana hasa katika kuhakikisha huduma zinaboreshwa hasa kwa kuongeza majengo na huduma mbalimbali kama hiyo ya dharura.
Amesema serikali ipo tayari kuunga mkono juhudi hizo hasa kwa kuhakikisha wahuduma wa afya wanaongezwa na vitendea kazi pia.
Akitoa taarifa fupi ya idara ya dharura mganga mfawidhi wa hospital Dokta Shafii Msechu amesema,ukarabati wa jengo la huduma za dharura limekaratabiwa kwa kushirikiana na taasisi ya Abbott Fund Tanzania.
Amesema lengo kubwa la kuanzisha idara hiyo ni kumaliza kabisa vifo vitokanavyo na magonjwa ya dharura na ajali.
Hata hivyo Dokta Msechu amesema mpaka sasa hospitali imeshakamilisha uchoraji wa michoro ya majengo ya waganjwa wa nje,jengo la dharura, jengo la wagonjwa mahututi na vyumba vya upasuaji.
Zaidi ya shilingi bilioni 9 zitatumika katika ujenzi wa jengo la dharura na shilingi bilioni 22 zitatumika katika ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje na jengo la dharura.
Akitoa shukrani za dhati makamu mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya Mt.Meru Hans Tosk, amesema bado hospitali inamahitaji mengi sana hivyo serikali na wadau wasichoke kuisadia hospitali pale mahitaji hayo yanapoombwa.
Pia, amesema bodi inafurahishwa sana na ushirikiano unaopatikana kutoka kwa serikali na kamshukuru sana Katibu Mkuu kwa kuwapa moyo wakuendelea kuboresha huduma za hospitali.
Huduma ya idara ya dharura kwa mara ya kwanza nchini ilizinduliwa rasmi katika hospitali ya Muhimbili 2010 na mafanikio makubwa yalionekana baada ya kupunguza idadi kubwa ya vifo,hivyo kupelekea idara hii kuanzishwa katika hospitali vyingine.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.