Jamii imehimizwa kutunza miundombinu ya miradi ya maendeleo kufuatia miradi inatekelezwa na fedha nyingi za Serikali sambamba na utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira.
Rai hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava muda mfupi kabla ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Maji Patandi eneo la Akheri Halmashauri ya Meru, wilaya ya Arumeru, mradi wenye thamani ya shilingi Bilioni 3.12.
Ndugu Mnzava amesema kuwa, Serikali inatumia fedha nyingi kutekeleza miradi ya maji, ikiwa na lengo la kusogeza huduma za maji karibu na wananchi ili kuhakikisha kila mwananchi anachota maji ndani ya eneo analoishi na kuongeza kuwa, wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo wa maji Patandi ambao hatua za utekelezaji wake unakwenda vizuri na kuwasisitiza wananchi kutunza miundombinu ya mradi huo, ili uweze kuwahudumia vizazi na vizazi.
Amewahimiza wananchi hao, kuizingatia utunzaji wa miundombinu hiyo ya maji, uende sambamba na utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira hasa kwa kuzingatia Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 inasisitiza autunzaji wa mazingira kwa maendelei endelevu.
"Dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama na ya uhakika, hivyo ni vema wananchi kumuunga mkono kwa kuitunza miradi ya maji na miundombinu yake, kutunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira na uoto wa asili, ili huduma hiyo ya maji iwe endelevu". Amefafanua Ndugu Mnzava.
Aidha Kiongozi huyo, ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo na kuweka Jiwe la Msingi huku akiwasistiza watalamu kuendelea kutekeleza mradi kadri Serikali inavyotoa fedha huku wakizingatia taratibu zote za utekelezaji wa miradi ya Serikali, ili uweze kukamilika na kufikia lengo la Serikali la kuhudmia wananchi kwenye maeneo yao.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu"
Mwenge wa Uhuru Oyeeeeeee
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.