• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

JAMII YASISITIZWA KUZINGATIA UMUHIMU WA LISHE KWA VIJANA BALEHE WA UMRI WA MIAKA 10 - 19

Posted on: October 30th, 2023

 Na Elinipa Lupembe

Jamii imesisitizwa kuzingatia umuhimu wa lishe bora kwa vijana wa rika balehe la miaka  10 -19 ambayo ni hatua muhimu ya ukuaji mara baada ya siku 1000 za mwanzo za maisha ya mtoto.

Rai hiyo imetolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya ya Lishe Mkoa Mkoa wa Arusha mwaka 2023, yaliyofanyika kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Meru, wilaya ya Arumeru.

Akizungumza kwa niaba Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John VK. Mongella, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Charles Rashid Mkombachepa,amesema kuwa suala la Lishe ni la muhimu katika afya ya binadamu lakini umuhimu unajikita zaidi kwenye hatua za makuzi ikiwemo hatua za makuzi kwa vijana wa rika balehe.

Amesema kuwa jamii inaoaswa kuzingatia lishe bora kwa vijana , kwa kuwa hatua ya ukuaji kwa vijana wa rika balehe, ndio maandalizi ya maendeleo ya mwili katika uzazi lakini maendeleo katika maandalizi ya nguvu kazi kwa  maenedeleo ya kijamii na kiuchumi.

"Lishe bora kwa vijana balehe ni muhimu kwa kipindi cha miaka 10 -19 ndio fursa adhimu ya ukuaji na maendeleo ya binadamu baada ya siku elfu moja za mwanzo wa maisha ya mtoto, hatua ambayo inamuandaa kijana kuwa nguvu kazi ya Taifa." Alisema Mkombachepa.

Aidha, ameeleza kuwa vijana balehe wana umuhimu wa kuzingatia lishe kwani ndio msingi wa maendeleo ya binadamu na ya Nchi, hivyo jamii kwa ujumla wake wanapaswa kuzingatia na kichukua hatua stahiki kuhakikisha vinaja wanapata lishe bora kwa afya zao.

Naye Mkuu wa Idara ya ya Afya Halmashauri ya Meru, Dkt. Evarist Chiweka, ameeleza kuwa Afya bora kwa vijana ni muhimu kwa kuwa ndio msingi wa nguvu kazi ya jamii na Taifa.

Aidha ameyataja madhara ya utapiamlo kwa wanawake na watoto wadogo ambao ndio wahanga wakubwa, unasababisha vifo kwa watoto wakati wa kujifungua, kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu na watoto ambao hawajafikisha muda wake(Njiti).

Naye Afisa Lishe Mkoa wa Arusha Dotto Milembe ameeleza  dhumuni la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa katika jamii,  kuhusu afya yanlishe na umuhimu wa lishe bora wa vijana hususani vijana wa rika balehe ambao ndio msingi wa nguvu kazi ya jamii na Taifa.

Ameyataja makadirio ya kidunia yanaonyesha kuna vijana Milion 1.2  wenye umri wa miaka 10-19 ambayo inaongezeka kwa kasi kubwa huku Tanzania ikikadiriwa kuwa robo ya watu wote ni vijana wa rika balehe.

Amesisitiza kuwa huduma za Afya ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za maendeleo ya Nchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 Sura ya 3 Ibara ya 81.

Iren Clement Makundi ni mwanafunzi kutoka  chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, amefurahi kushiriki katika maadhimisho hayo kwani amejifunza umuhimu wa lishe bora kwa vijana balehe.

" Nimeokolewa na elimu finyu iliyokuwepo katika kichwa changu kwani leo nimeelewa umuhimu wa lishe bora kwa kijana hasa wakati wa kupevuka" Alisema Iren.

Awali maadhimisho hayo mkoa wa Arusha, yameambatana na utoaji wa huduma bure za Afya, ikiwemo upimaji wa hali ya lishe, ulinganisho  wa Urefu na Uzito pamoja na kutoa elimu ya vyakula ya Afya na lishe yakiwa yamebeba Kauli Mbiu ya " Lishe bora kwa Vijana balehe ni chachu ya mafanikio yao"

Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.