Wananchi wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuchukua tahadhari na hatua zote za kujinga na ugonjwa wa Covid 19.
Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Arusha DC, Meru, Longido na Monduli waliowawakilisha Halmashauri zingine za Mkoa.
Amesema tahadhari hiyo izingatiwe na wananchi wa Mkoa mzima wa Arusha na katika maeneo mbalimbali kama vile Makanisani, Misikitini, Masokoni na maeneo yote ya mikusanyiko.
RC Mongella amesema ugonjwa huo si wakupuuzia kwani ni kwa ajili ya maisha ya wananchi hao.
"Hata kama maambukizi bado yapo chini hatupaswi kupuuzia hata kidogo,alisema".
Amezitaka ofisi zote za Serikali kuhakikisha watu wote wanavaa Barakoa, wana nawa Mikono na Maji tiririka au vitakasa mikono na kuepuka mikusanyiko.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ametoa maelekezo hayo baada ya wananchi wengi kupuuzia tahadhari zilizokwisha tolewa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.