Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Festo Shemu Kiswaga, amehimiza wananchi wa mkoa wa Arusha, kujioa kushiriki katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira, kwa kuwa ni jukumu la kila mwanajamii.
Mhe. Kiswaga ametoa rai hiyo, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti Mkoa wa Arusha, yaliyofanyika kwenye shule ya Msingi Emairete, kijiji cha Emairete kata ya Monduli Juu, wilaya ya Monduli, leo Aprili 03, 2024.
Maadhimisho ya Upandaji miti hufanyika kila mwaka, huku mwaka 2024 yakibeba Kauli Mbiu ya 'Misistu na Ubunifu'.
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.