Jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mtu, sio kwa vyombo vya ulinzi na usalama pekee hasa katika maeneo yetu.
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella alipokuwa akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Posmolu na Ololosokwani Wilaya ya Ngorongoro.
" Kwa Sasa hali ya ulinzi na usalama ni nzuri katika eneo hili la mpaka,lakini tusibweteke tuendelee kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama".
Kila Mwananchi ni mlinzi wa kwanza katika eneo lake, hii itasaidia kuleta amani na usalama wa kila mtu.
Amewataka wananchi hao kutoa taarifa mara moja pale wanapohisi hali ya uvunjifu wa amani katika vijiji hivyo.
RC Mongella amefanya ziara katika mpaka, kati ya Tanzania na Kenya katika Kijiji cha Posmolu Wilayani Ngorongoro.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.