Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu wametakiwa kufanya kazi kwa juhudi huku wakizingatia utoaji huduma kwa weredi,ushirikiano na utunzaji wa Siri.
Yamesemwa hayo na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo, katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
"Nataka kila Mkuu wa idara afanye kikao na watumishi wake kwenye idara kila mwezi na kupeleka taarifa CMT, hii itasaidia kuwa na uwazi wa mambo yote".
Aidha amekemea vikali vitendo vya rushwa kwa watumishi kwani vinasababisha kupunguza weredi katika kazi.
Amewataka watumishi hao kuwa na mpango kazi kwa kila mtu ili kuwawezesha kuyafahamu majukumu yao na kuongeza ufanisi.
Nae, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Mhe.Rajabu Kalia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri hiyo fedha nyingi za miradi ya maendeleo.
Dkt. Kihamia amefanya kikao na watumishi wa Halmashauri ya Karatu, ikiwa ni uratibu wa kawaida wa kikazi kuwakumbusha watumishi hao majukumu yao.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.