Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imeunda kamati maalumu 115 za kufuatilia kwa karibu viashiria na kukomesha matukio ya ukatili wa kijinsia kwa Watoto na wanawake katika jamii.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange wakati akichangia hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Makundi Maalumu ambapo amesema kamati hizo zitahakikisha zinatoa elimu kuanzia ngazi ya mitaa na vijiji.
“mpaka sasa elimu na hamasa ambazo zimetolewa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ni midahalo 4,748 katika maeneo mbalimbali nchini na midahalo hiyo ilikuwa ni mahususi kwa kuonesha ukubwa wa tatizo na kutoa elimu na hamasa ili kila mmoja awe mlinzi wa mtoto na kila mmoja awajibike kutoa taarifa katika vyombo vya sheria” amesema Dkt. Festo Dugange
Katika kusisitiza hilo Dkt. Dugange amesema tayari imeshafanyika mikutano 61,387 yakujadili masuala mbalimbali ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kuwezesha viongozi na jamii kutambua ukubwa wa tatizo na kuchukua hatua ya kudhibiti changamoto hiyo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.