Na Elinipa Luoembe
Kamati ya Kudumu ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, imewasilia mkoani Arusha kwa ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na kwa fedha za uendeshaji wa Mjiji na Majiji nchini ( TSCP).
Wakiwa mkoani Arusha wajumbe hao watatembelea utekelezaji wa mradi wa katika eneo la kuhifadhi taka ngumu 'Dampo' kata ya Muriet pamoja na miundombinu ya barabara kuingia na kutoka Jiji la Arusha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge TAMISEMI Mhe. Denis Lazaro Londo (MB) amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kutembelea miradi ya uboreshaji wa Miji na Majiji ni kujionea maendeleo ya mradi ili kubaini changamoto ikiwa ni maandalizi ya utekelezaji wa mradi mkakati unaokuja wa kuboresha hadhi za Miji na Majiji 'Tanzania Cities Transforming Infastructure & Competitiveness Project' (TACTIC).
"Tumetembelea halmashauri nne ikiwemo za Jiji mbili na Manispaa mbili ambazo ni wanufaika wa mradi wa TSCT ili kufahamu maendeleo yako ikiwa ni mwelekeo wa mradi unaotarajiwa kuanza wa kuboresha hadhi za Miji na Majiji nchini" Amesema Mwenyekiti huyo
Hata hivyo Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi amesema, kupitia mradi wa TSCP kamati itapata uwelewa wa pamoja utakaokuwa dira ya utekelezaji wa mradi wa awamu ya pili wa kuboresha Majiji wa TACTIC kwa kuwa miradi hii ndio miradi ya kimkakati inayofuata baada ya hii kukamilika.
Ameweka wazi kuwa serikali ya awamu ya sita inategemea kuanza awamu ya pili ya kuetekeleza miradi mkakati ya kuboresha Miji na Majiji kwenye halmashauri 12, Jiji la Arusha liwa miongoni mwao kwa ufadhili wa Benki Kuu ya Dunia, ikihusisha ujenzi wa masoko, vituo vya mabasi pamoja na miundombinu ya barabara.
"Moja ya eneo lililopata fedha nyingi ni Jiji la Arusha, kwa kuwa kila mtu anafahamu idadi kubwa ya wageni wanaoingia na kutoka kupitia Arusha kwa shughuli za utalii, uchumi na uatawala" Amesema Mhe. Ndejembi
Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella licha ya kuwakaribisha wajumbe hao wa Kamati ya Kudumu ya Bunge TAMISEMI na kuwahakikishia usalama wa mkoa wa Arusha amewashukuru kwa kupata fursa ya kupitia utekelezaji wa maendeleo ya Jiji la Arusha kwa kuwa usimamizi wa miradi ndio nyenzo ya maendeleo ya Taifa letu.
Amesema kuwa, kwa sasa kuna uwekezaji mkubwa unaendelea katika mkoa wa Arusha ukihusisha viwanda, kilimo, ufugaji na madini huku utalii ukiwa ndio muhimili wa uchumi wa wananchi wa mkoa huo, na kuongeza kuwa mradi wa TSCP umewezesha uwepo wa miundombinu rafiki unaochochea ukuaji wa kasi wa maendeleo ya kiuchumi.
Aidha amemshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuhamasisha utalii kupitia Filamu ya Royal Tour, programu ambayo imeleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya utalii ikiwa ndio muhimili wa uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.
"Mradi unaokuja wa kuboresha majiji awamu ya pili (TACTIC) utachangia ukuachi wa uchumi katika sekta zote hususani sekta nyeti ya utalii, mwaka huu msimu wa utalii umeunganisha tunapokea idadi kubwa ya watalii karibu mwaka mzima, mkakati wetu kama mkoa ni kuhimiza uwekezaji katika sekta ya utali kwa kuwa na uhitaji mkuwa wa maeneo ya malazi yatakayokuwa na hadhi kuwakarimu wageni wanaofika Arusha"Amebainisha Mhe. Mongella
#Arushafursalukuki
#KaziInaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.