Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, wametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni na miundombinu ya vyoo, shule ya sekondari ya Wasichana Arusha, iliyopo mtaa wa Oleresho Kata ya Olasiti, Jiji la Arusha, wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika sekta ya Elimu leo Februari 26, 2024
Mradi huo uliojumuisha ujenzi wa vyumba 15 vya Madarasa, Mabweni 02 na matundu 21 na kugharimu shilingi milioni 679.1 kwa ufadhili wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation
Vyumba 15 vya madarasa 15 vimegharimu shilingi milioni 375, milioni 260 zikijenga mabweni mawili yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 160, wanafunzi 80 kwa kila bweni huku matundu ya vyoo yakigharimu shilingi milioni 44.1.
Shule ya mchepuo wa Sayansi ina jumla ya wanafunzi 354 kati yao kidato cha Tano wapo 247 na kidato cha Sita ni 107, ikiwa na tahasusi 4 za PGM, PCM, EGM na HGE. Shule hii ni ya mchepuo wa sayansi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.