Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha wametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Sinya na kuutaka uongozi wa shule hiyo, kuotesha miti kuzunguka maeneo yote ili kutunza mazingiraa na uoto wa asili.
Hata hivyo akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Thomas Ole Sabaya, licha ya kupongeza mradi huo ambao umekamilika na wanafunzi kuanza masomo ameutaka uongozi wa shule hiyo kuboresha mazingira kwa kupanda miti inayoendana na maeneo hayo ili kupata kimvuli kwa walimu na wanafunzi kutokana na eneo hilo kuwa na vipindi vya joto wakati mwingi.
Awali, mradi huo umetekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 570 kupitia miradi ya SEQUIP.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.