Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Loy Thomas Ole Sabaya, wamepongeza utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa shule mpya ya sekondari Sekei kata ya Sekei jiji la Arusha, mradi ambao umetekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 584. 2, fedha kutoka Serikali Kuu, kupitia mradi wa kuboresha mindombinu ya shule za sekondari SEQUIP.
Wajumbe hao kwa pamoja waupongeza uongozi wa mkoa kupitia halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuamilisha ujenzi wa shule hiyo kwa wakati na hatimaye wanafunzi 95 waliopangiwa kuanza kidato cha kwanza wakiwa darasani, huku mradi huo ukiwa na viwango vya ubora vinavyoendana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.
Mwenyekiti wa UWT CCM mkoa wa Arusha, Florah Zelothe, amewapongeza kwa usimamizi imara wa fedha za umma na hatimaye kukamilisha mradi kwa kipindi kifupi, mradi ambao thamani ya pesa na ubora wa mradi vinaonekana kwa macho huouzuri wa mradi huo, wenye mindombinu ya kisasa
Aidha wamewataka walimu, kuwasimamia wanafunzi ili kuitunza miundombinu na samani zake ili zidumu kwa muda mrefu pamoja na kutunza mazingira ya nje kwa kupanda miti, kuzunguka eneo lote la shule.
Awali, akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mkuu wa shule ya Sekondari Sekei Mwl. Joshua Kisivan Mollel amasema, mradi huo umetumisa shilingi milioni 584.2 ukijumuisha ujenzi wa jengo la utawala, vyumba nane vya madarasa, maabara tatu za masomo ya Sayansi ikiwemo Kemia,Biolojia na Fizikia, Maktaba, jengo la TEHAMA, pamoja na matundu nane ya vyoo vya wasichana na wavulana.
Amsema Shule hiyo imesajiliwa kwa namba ya usajili S.6448 na tayari imepokea wanafunzi 96 wa kike 50 na wa kiume 46 na ugundishaji umeanza tangu Januari 08, 2024 kufuatia ratiba ya mwaka wa masomo ulioanza 2024.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.