Wajumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha, wametembelea na kukagua miradi shule ya Sekondari Amsha, kata ya Ambureni, halmashauri ya Meru, wilaya ya Arumeru na kuuagaza uongozi kukamilisha miradi yote viporo mpaka kufikia kufikia Aprili 2024.
Maagizo hayo yamekuja baada Kamati hiyo kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu, jengo la utawala na maabara ya masomo ya Sayansi, miradi ambayo inayotekelezwa na fedha za Mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Loy Ole Sabaya amesema kuwa, kumekuwa na miradi mingi viporo katika shule hiyo, miradi ambayo imezua malalamiko mengi miongoni mwa wananchi inayotokana na kutokuelewana miongoni mwao, na kuwasisitiza kukamilisha miraci hiyo ifikapo mwezi Aprili, 2024 ili kuondoa malalamiko yaliyopo.
Hata hivyo, Mwenyekiti Sabaya amewataka wananchi hao, kuachana na malumbano kwa kuwa yanachelewesha na kurudisha nyuma maendeleo na kuwasihi kusikilizana na kunia mamoja ili kwa kuwa, kwa sasa lengo la serikali na watanzia ni maendeleo na sio malumbani.
"Wananchi wa Ambureni, wacheni malalamiko na malumbano yasiyokwisha, kama malalamiko yalishatolewa maamuzi ni vyema kuwachana na mambo ya zamani na kuanza upya kwa ajili ya maendeleo ambayo ndio lengo la Serikali, kaeni pamoja kubalieni" Amesema Sabaya
Awali, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe.John V.K Mongella, ameahidi kusimamia utekelzaji wa maagizo hayo ya kamati ya Siasa kwa kumtaka Mkurugenzi wa halmasahuri ya Meru kuhakikisha miradi yote viporo shuleni hapo inakamilika, ikiwa na viwango vya ubora vilivyokulika kulingana na thamani ya fedha.
"Miradi hapa imechelewa na wapo ambao walihujumu na kutumia fedha vibaya, ninakuagiza Mkurugenzi hakikisha miradi inakamilika yote huku majengo yote yakiwa yamewekwa sakafu ya malumalu 'tiles' kama yalivyo makubaliano yetu ya mkoa kwenye miradi yote".Amesema Mhe. Mongella
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.