Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha imetembelea na kukagua jumla ya miradi 4 yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.56 katika halmashauri ya wilaya ya Karatu, Machi 09, 2024.
Wajumbe hao wa Kamati ya Siasa Mkoa wakiongozwa na Mwenyekiti w CCM Mkoa wa Arusha, Loy Thomas Ole Sabaya, wamekagua mradi wa ujenzi shule mpya ya sekondari Lake Eyas kata ya Mongola, Mradi wa Ujenzi wa ahule mpya ya Sekondari Laja kata ya Kansay, Mradi wa Umeme wa REA kitongoji cha Maurus kata ya Endabash na Ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya sekondari Ayalabe, kata ya Ganako.
Wakiwasilisha taarifa za miradi hiyo, watalamu wasimamizi wa miradi kisekta kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Dadi Horace Kolimba, wamefafanua kuwa, Mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Lake Eyasi, umetekelezwa kwa gharama ya shilingi Milioni 584.2, na ujenzi wa nyumba ya walimu yenye sehemu ya kuishi familia mbili (2 in 1) uliogharimu shilingi Milioni 98, fedha zote kutoka Serikali Kuu, kupitia mradi wa Kuboresha Miundombinu ya Shule za Sekondari Nchini (SEQUIP).
Mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Laja, umetekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi Milioni 333.3 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF OPEC IV.
Aidha, Kamati imekagua pia mradi wa Umeme katika Mgodi wa Dhahabu wa Endagem, uliogjarimu kiasi cha shilingi milioni 545.3 kupitia Wakala wa Nishati Vijijini REA, umeme ambao umefikishwa kwenye eneo la mgodi huo kitongoji cha Maurus.
Hata hivyo, wajumbe wa kamati hiyo ya Siasa wamerishishwa na hali ya utekelzaji wa miradi hiyo licha ya changamoto ndogo zilizoonekana na kuzitolea maagizo, lakini wameipongeza Serikali ya Awamu ya sita, kupitia Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, watalamu, viongozi wa ngazo zoye pamoja na wananchi, kwa kujitoa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo kwa kuhakiksha miundombinu ya kutolea huduma za jamii, imewafikia wananchi katika maeneo yao.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.