• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

KAMISHNA KIIZA ASHIRIKI ZOEZI LA KUELIMISHA WANANCHI WANAOTAKA KUHAMA KWA HIARI NGORONGORO.

Posted on: March 7th, 2024


Na Mwandishi wetu, Ngorongoro.


Kamishna wa uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Richard Kiiza amefanya ziara katika baadhi ya vijiji vilivyoko ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kukagua maendeleo ya timu ya uelimishaji na uandikishaji wa wananchi wa tarafa ya Ngorongoro wanaojiandikisha kuhama kwa hiari ndani ya hifadhi hiyo.


Akiwa kwenye ziara katika Vijiji vya Kayapusi na Oloirobi vilivyopo kata ya Ngorongoro, Kamishna Kiiza amekutana na moja ya timu inayoendelea na zoezi la uandikishaji na kuelezwa kuwa wananchi wameendelea kuhamasika na kujiandikisha kwa hiari hasa baada ya kupata elimu ya faida na hasara za kuishi ndani ya hifadhi na kupata taarifa za fursa lukuki za ndugu zao waliokwisha hama ndani ya hifadhi.


Akizungumza na baadhi ya wananchi aliokutana nao Kiiza amewaeleza kuwa Serikali hailazimishi mtu kuhama isipokuwa inamuelimisha hasara za kuishi ndani ya hifadhi ambapo sheria inazuia kufanya baadhi ya vitu ukilinganisha na mazingira anakoenda ambapo serikali imeboresha mazingira kwa kujenga miundombinu ya maji, shule, barabara, umeme, mawasiliano, eneo la malisho, minada na soko la maziwa.


Ameongeza kuwa wananchi ambao wangependa kwenda kuona maeneo yaliyoandiliwa na Serikali kabla ya kuamua kuhamia wana uhuru wa kufanya hivyo ili  kukagua maeneo yaliyoandaliwa katika vijiji vya  Msomera, Kitwai na Saunyi na serikali ipo tayari kuwapa ushirikiano.


“Serikali haiwezi kuwa na nia mbaya kwa watu wake, ndio maana inajenga miundombinu yote muhimu, inawapa wananchi wanaohama fedha za motisha zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, sambamba na kuwapa fidia ya maendelezo waliyofanya wakiwa ndani ya hifadhi na kuwahamishia thamani na mifugo yao yote kwenda maeneo waliyochagua  kwa kufuata misingi ya sheria, kanuni na haki za binadamu” amefafanua Kiiza.


Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO MTIHANI WA UTAMIRIFU (MOCK) 2025 DARASA LA SABA (VII)- MKOA WA ARUSHA June 07, 2025
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • KARIBU ARUSHA Mhe. KENAN LABAN KIHONGOSI MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    June 26, 2025
  • KARIBU ARUSHA Mhe. KENAN LABAN KIHONGOSI MKUU WA MKOA WA ARUSHA

    June 26, 2025
  • SIKU YA KWANZA; WAKAZI WA ARUSHA WAJITOKEZA KWENYE KAMBI YA MADAKTARI BINGWA NA MABINGWA WABOBEZI

    June 23, 2025
  • RC MAKONDA ASHIRIKI MARATHON YA KKKT 2025

    June 21, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.