Siku moja baada ya uzinduzi wa filamu ya “Amazing Tanzania” (Mailii Tansaniya) iliyomshirikisha Rais Dakt. Samia Suluhu Hassan na msanii wa China, Jin Dong, uliofanyika jana kwenye ukumbi wa National Opera House jijini Beijing, kampuni za China zimeendelea kuchangamkia fursa za ushirikiano zaidi na Tanzania katika sekta mbalimbali.
Leo Mei 16, 2024, kampuni ya Kichina ya Touchroad imetangaza kuleta watalii watakaoambatana na wasanii mashuhuri wa China kuja Tanzania mwezi ujao kufanya utalii na kuitangaza zaidi Tanzania huku kampuni hiyo pia ikiahidi kuratibu shindano kubwa la kimataifa la mbio ndefu (marathon) Zanzibar na Dar es Salaam kuanzia mwezi ujao.
Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Beijing katika mkutano wa pamoja kati ya uongozi wa kampuni hiyo na viongozi wa Tanzania wakiongozwa na mawaziri Angellah Kairuki wa Utalii na Damas Ndumbaro wa Michezo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.