KAMPUNI YA SANKU YATEKELEZA MKAKATI WA UPATIKANAJI WA LISHZ BORA KWA JAMII
Serikali kwa kushirikiana na kushirikiana na wadau wa Shirika lisilo la Kiserikali la SANKU, wanatekeleza mkakati wa kuhakikisha upatikanaji wa lishe ya uhakika kwa Watanzania kwa kusambaza mashine maalumu za kusaga nafaka na kuziongezea virutubisho kwenye Mikoa yote nchini.
Kupitia programu hiyo, Shirika hilo limefanikiwa kugawa mashine maalum za kuchanganya virutubisho kwa uwiano unaohitajika kulingana na viwango vya lishe vinavyohitajika kwa matumizi ya binadamu, lengo likiwa ni kupambana na utapiamlo hususani kwa watoto.
Akizungulza wakati wa kufunga mashine hiyo kwenye shule ya msingi Mundarara wilaya ya Longido, Meneja Mwandamizi Kampuni ya SANKU, Gwao Omari Gwao, amesema kuwa, Kampuni hiyo inatekeleza mradi huo kwenye mkoa wa Arusha kwa kufunga mashine hizo kwenye viwanda binafsi na vya Umma, vinavyosindika unga mahindi na kufungusha
"Mshine hizo zinachangaya virutubisho vya madini ya Zinki, Vitamin B 12, asidi ya foliki, na madini ya chuma kwenye nafaka mahindi, kwa uwiano sahihi wakati wa kusaga, ili kupata lishe kamili, kwa kuwa watanzania wengi wanashindwa kupata mlo kamili wenye virutubishi vyote kutokana na kipato duni" Amefafanua Gwao
Aidha, Gwao ameweka wazi kuwa, katika mkoa wa Arusha SANKU imefanikiwa kufunga mashine hizo kwenye viwanda 20 huku mashine 7 zikifungwa kwenye shule za msingi na sekondari katika halmashauri zote 7 za Mkoa wa Arusha.
Hata hivyo, Wananchi wa Mundarara wameishukuru Serikali kupitia SANKU, kwa kutekeleza mkakati huo wa kuboresha lishe kwa afya za wananchi na kuwapelekea mashine ambayo itawasaidia hasa watoto wao kupata lishe bora shuleni na kuahidi kuhamasisha wananchi wote kutambua umuhimu wa lishe bora hususani kwa akina mama wajawazito na watoto.
"Ili kuhakikisha kuwa tunaunga juhudi za Serikali za kuboresha afya za wananchi wake, tutahakikisha tunatoa elimu kwa wananchi wote waelewe umuhimu wa Lishe bora na kuzishawishi shule jirani kutumia mashine hii kwaajili ya chakula cha watoto". Amesema Mhe. Alex Reuben, Diwani wa kata ya Mundarara.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.