Waziri wa Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amewataka wananchi wote kuhakikisha wanaweka mazingira yao safi na salama wakati wote.
Ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya Malaria Kitaifa Mkoani Arusha na akizindua mpango mkakati wa kudhibiti Malaria kwa Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Dkt. Gwajima amesema njia liliyobora ya kupambana na Malaria ni kila mmoja kuchukua hatua za kupambana nayo ikiwemo kutumia vyandalua vyenye dawa, kunyunyuzia viwatilifu koko katika kuta za Nyumba.
Pia, kuuwa viwatilifu wadudu katika mazingira ya wananchi na wajawazito kutupia ASP.
Kiwango cha Malaria kimeshuka kwa 50% kwa sasa nchini kwani mwaka 2015 kilikuwa 14.5% na 2017 ni 7.5%.
Hivyo kufanya kiwango cha maambukizi kwa Tanzania bara ni 24.4%, hususani katika Mikoa ya Kigoma 24%, Geita 17%, Kagera na Mtwara 15%.
Mikoa ambayo inamaambukizi ya Malaria kwa kiwango cha chini ya 1% ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Iringa na Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Hassan Kimanta amesema Mkoa wa Arusha umeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa chini ya 1% hadi kufikia mwaka 2020.
Aidha, idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Malaria vimepungua kwa 80% kutoka vifo 20 kwa mwaka 2015 hadi vifo 4 mwaka 2020.
Pia, idadi ya wagonjwa imepungua kutoka wagonjwa 15150 mwaka 2015 hadi 9314 mwaka 2020 sawa na punguzo la 35%.
Kimanta amesisitiza kuwa mpango mkakati wa Mkoa wa Arusha ni kutokomeza ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030.
Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani huadhimishwa kila ifikapo Aprili 25 na kwa mwaka huu 2021 Kitaifa yamefanyika katika Mkoa wa Arusha na kuzindua mpango Mkakati wa kutokomeza Malaria nchini ifikapo 2025 kwa 3%.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.