Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akiwa na vijana wa mkoa huo ambao wanatoa burudani mbalimbali wakiwemo waendesha pikipiki kwa ustadi wa kiburudani, wakati wa Mkesha wa mwaka Mpya leo Desemba 31, 2024
Mkesha huo umepambwa na burudani mbalimbali ikiwemo mbio za Farasi, Pikipiki pamoja na mbio za magari, suala ambalo limekuwa kivutio kikubwa kwa mamia ya wananchi wa Mkoa wa Arusha na mikoa mingineyo ambao wamefika Mkoani Arusha kwaajili ya kusherehekea Ukaribisho wa mwaka 2025.
Sherehe hizi ambazo zinaingia siku yake ya tatu na ya kilele, inaratibiwa na kusimamiwa na Mhe. Makonda.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.