Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Bohora mkoa wa Arusha, Sheikh Idris Imram Ally amefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. John V.K Mongella kwa lengo la kujitambulisha na kusaini kitabu cha wageni, leo 18 Januari, 2024.
Kiongozi huyo aliyepangiwa kushika nafasi, akitokea nchini India, baada ya Kiongozi aliyekuwepo Sheikh Aliasger Qamos, kumaliza muda wake na kupangiwa majukumu mengine, amejitambulisha kwa uongozi wa mkoa ili kutambua uwepo wake na kuomba ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake mkoani hapo.
Awali, Kiongozi huyo amembatana na viongozi wengine wa dhehebu hilo, licha ya kujitambulisha, wamemkabidhi zawadi ya mwaka mpya 2024 Mkuu wa Mkoa, kwa niaba ya Sheikh Mkuu aliyepo Nchini India, ikiwa ni ishara ya upendo na ushirikiano baina ya uongozi wa mkoa na dhehebu hilo la Bohora.
Hata hivyo, Mhe. Mongella amemshukuru na kumkaribisha Kiongozi huyo nchini Tanzania hususani Mkoani Arusha na kumuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake ya kazi na kumtaka kufurahia mandhari na hali ya hewa nzuri ya mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.