Kufuatia mpango wa Serikali ya awamu ya sita wa kusogeza miundombinu ya maji kwenye maeneo wanayoishi wananchi, Serikali imetekeleza mradi wa maji wa Chemchem uliogharimu shilingi milioni 590, ambao umetegua kitendawili cha upatikanaji wa maji safi na salama kijiji cha Chemchem kata ya Rotia wilaya ya Karatu.
Kitendawili hicho kilepata majibu sahihibaada ya Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa 2024, Ndugu Godfrey Eliakimu Mnzava kutembelea mradi huo wa maji uliozinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 kuzindua mradi huo ambao ni ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 135,000 na vituo 18 vya kuchotea maji na birika la kunyweshea mifugo, mradi ambao umewafikia jumla ya wanachi 6,000 wa kijiji hicho cha Chemchem.
Akizindua mradi huo, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, ameweka wazi kuwa mradi huo umeleta majawabu ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan majibu ambayo wananch8 waliyatamani kwa muda mrefu.
Malengo ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi na salama ndani ya maeneo yao kufuatia programu ya kumtua mama ndoo kichwani.
Mnzava amepongeza RUWASA kwa kutekeleza mradi vizuri uliokidhi vigezo vinavyoendana na thamani ya fedha kwa kutumia mfumo wa manunuzi wa kielektoniksi (NeST) na kuunda Jumuia ya watumia maji na kusisitiza kuwa Jumuia hiyo CBWSO waendelee kusimamia kwa uaminifu, ugawaji wa maji.
"Tumeshuhudia baadhi ya maeneo kuna changamoto ya ugawaji usio na usawa, niwasihi Jumuia hii kugawa maji kwa usawa bila upendeleo, tunahitaji mgao uwe na usawa kila mtu anahitaji kupata maji maji kwa kuwa hayana mbadala wake". Amesema
Hata hivyo, amewataka wananchi kuwa usimamizi wa Jumuia ya Watumia maji ngazi ya jamii, kutunza miundo mbinu hiyo ya maji, ili iweze kudumu na kuhudumia kwa miaka mingi ijayo.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni "Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu"
Mwenge wa Uhuru Oyeee
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.