Kamishina Jenerali wa Magereza Mzee Ramadhani Nyamka amesema kuwepo kwa kituo cha kushikilia watuhumiwa na wafungwa wa mauwaji ya Kimbari kilichokuwa kikisimamiwa na Umoja wa Mataifa kimeleta faida kubwa kwa baadhi ya maafisa wa polisi kuongeza ujuzi katika utendaji wao wa kazi.
Ameyasema hayo alipokuwa akipokea kituo hicho kwa niaba ya Serikali kutoka kwa Msajili wa Mahakama ya Masalia ya Kesi ya mauwaji ya Kimbari Abubacarr Tambadou.
Amesema kurudishwa kwa kituo hicho kwa Serikali ya Tanzania kutasaidia kupunguza msongamano katika magereza ya Tanzania kwani baadhi ya wafungwa watahamishiwa katika kituo hicho.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema kituo hicho kitasaidia kuongeza uwezo kwa Gereza la Kisogo.
Aidha, amesema Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na mfumo wa Magereza kuhakikisha eneo hilo linasimamiwa vizuri.
Kituo cha kushikiria watuhumiwa na wafungwa wa mauwaji ya Kimbari kilianzishwa Mkoani Arusha mwaka 1996 chini ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.