• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

KONGAMANO LA KWANZA LA WANAMIPANGO MWAKA 2023, LAFANYIKA ARUSHA; RC MONGELLA AWAKARIBISHA ARUSHA..

Posted on: November 27th, 2023

Na Elinipa Lupembe.


Kongamano la kwanza la Wanamipango nchini mwaka 2023, linafanyia mkoani Arusha, mara baada ya Serikali ya awamu ya Sita, kurejesha Wizara ya Mipango na Uwekezaji, chini ya Ofisi ya Rais, na kufunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (MB), kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha


Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K.Mongella ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kurejesha, Tume ya Mipango na Uwekezaji huku Kongamano la kwanza la Wanamipango nchini likifanyika Mkoani Arusha na kuipongeza, Wizara ya Mipango na Uwekezaji kwa kuchagua Mkoa wa huo kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo.


Mhe. Mongella amekiri kutambua umuhimu wa kupanga kuanzia ngazi ya mtu binafsi, familia, Taasisi hadi Taifa, mipango inayowezesha kutoa huduma, kulingana na uhitaji ili kuleta maendeleo na kuongeza kuwa, amekuwa akiwasisitiza wataalam wa Mkoa na ngazi zote za Arusha, kuhakikisha wanakuwa na mipango ya pamoja inayotekelezeka ili kuleta maendeleo kwenye jamii zinazohudumiwa.


"Binafsi ninaamini kushindwa kupanga ni kupanga kufeli, kwa kuzingatia hili, kila Mwana mipango analo jukumu la kuimarisha mipango inayozingatia mahitaji ya jamii na rasilimali zilizopo"


Aidha, ameutaja umuhimu wa Kongamano hilo, likiwa  limekusanya Wataalam na Wadau wa mipango kutoka sehemu mbali mbali za nchini, wakiwa na lengo la kujengeana uwezo na kutengeneza mfumo mzuri wa upangaji kwa maendeleo ya Taifa letu.


Aidha ametumia fursa hiyo, kuwakaribisha Wanamipango mkoani Arusha, mkoa ambao ni kitovu cha Utalii na kuwataka, washiriki kutembelea vivutio vya utalii ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais za kukuza utalii nchini na kuwahakikishia usalama wa washiriki wote kwa kipindi chote watakapo kuwa mkoani hapo.


"Kwa niaba ya wananchi wa Arusha, na Uongozi wa Mkoa, tupo tayari kutoa ushirikiano muda wote tutakapohitajika, ninawasihi washiriki mpatapo nafasi msisite kutembea kujionea mandhari nzuri ya Mkoa wetu" Amesema Mhe. Mongella.


Kongamano la  Wanamipango mwaka 2023, limefunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (MB), linalofanyika kwa siku 4, kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC), lenye Kauli Mbiu ya "Fikra za Pamoja na Utekelezaji, Ulioratibiwa kwa Ustawi Jumuishi"




Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.