Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema lengo la zoezi la upandaji Miti ni kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu katika juhudi za kutunza mazingira.
Ameyasema hayo alipokuwa akihitimisha maadhimisho ya miaka miwili ya Rais Samia tokea akiwa madarakani.
Kupitia jitihada alizofanya za kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya nchi yetu.
Pia, ameweza kujenga Madarasa yakutosha ili kuwaweza wanafunzi wawe na mazingira mazuri yakusoma.
Ameweza pia kukuza Demokrasia ya Mahusiano ya Kimataifa kwa kuitambulisha nchi.
Kwa upande wa Mkoa wa Arusha katika miaka hii 2 fedha za miradi ya maendeleo iliyotolewa na Halmashauri ni takribani Bilioni 50 sawa na 86.9%, ngazi ya Mkoa Bilioni 2.5 zilipokelewa kwa ajili ujenzi wa Nyumba za Maafisa Tarafa.
Sekta ya afya ilipata Bilioni 27.5,Sekta ya Elimu ilipata Bilioni 24.4, Sekta ya Maji (RUWASA) wamepokea Bilioni 11.8,katika Sekta ya Umeme jumla ya Vijiji 290 kati ya 394 vimeshapatiwa umeme na kiasi cha Bilioni 58.9 zimepokelewa kwa ajili yakuendelea kusambasa umeme maeneo mbalimbali.
Vile vile katika sekta ya Barabara (TARURA) wamepokea fedha Bilioni 42 kwa ajili ya kutengeneza barabara mbalimbali,TANROADS nao walipokea Bilioni 586.9.
Serikali ya awamu ya Sita katika kuwawezesha wananchi kiuchumi (TASAF) Mkoa ilipokea Bilioni 30.9 na miradi mbalimbali imeweza kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa Madarasa, Mtundu ya vyoo, Mabweni, Mabwalo ya chakula, Ofisi za Walimu na Nyumba zao.
RC Mongella amesema kwa juhudi hizo za Mhe.Rais Samia Mkoa wa Arusha unajivunia mafanikio makubwa sana hasa katika Sekta ya Utalii imekuwa kwa kiasi kikubwa kutokana na Filamu ya "The Royal Tour" iliyofungua milango ya watalii wengi kuja Mkoani humo.
Maadhimisho ya miaka 2 ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwepo madarani, Mkoa wa Arusha umeadhimisha kwa wiki nzima ambapo yalizinduliwa 13 Machi,2023 kwa kuzindua Kitabu kilichoelezea mafanikio ya miaka miwili, ikifiatiwa na shughuli mbalimbali za michezo na kuhitimishwa 19 Machi, 2023 kwa zoezi la upandaji Miti.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.