Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kushurikiana na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania katika kuhudumia mwananchi.
Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Viongozi pamoja na waumini wa Kanisa hilo katika maadhimisho ya miaka 60 ya kanisa hilo.
Rais Samia amesema swala la uwalibifu wa mazingira yametokana na sisi wenyewe kushindwa kuwa rafiki kwa mazingira na yanatuadhibu wenyewe.
Amesisitiza kuwa hatua zilichokuliwa na Serikali katika kutunza mazingira ni matumizi ya solar kule Shinyanga na umeme wa upepo kule Tabora ili kutunza mazingira.
Kutokana na uharibifu wa mazingira umepelekea kuwa na tatizo la usalama wa chakula na nchi yetu ya Tanzania bado tunaendelea kuzalisha chakula bora kinacholisha maeneo mengi.
Amewataka viongozi watakaochaguliwa kwenda kuendelea kusimamia misingi ya kanisa ikiwemo umoja na mshikamano ambao ndio unaenda hadi kwenye nchi.
Amewataka viongozi wote wa kidini kukuza ,kusimamia na kuenzi maadili yetu ili watoto wetu wawezi kuyaishi na kuwakuza katika maadili hayo.
Amelitaka Kanisa la kijidhatiti kwa kuangalia mabadiliko yanayotoke Duniani na katika nchi nakuweza kuendana nayo hasa yale mazuri ili kuleta maendeleo.
Nae,Askofu Mkuu wa Kanisa kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Fedrick Shoo amesema kanisa hilo limeanza mwaka 1963 na waumini takribani 5000 hadi kufikia waumini takribani milioni 8 kwa sasa na jiyo ikiwa ni muungano wa makanisa 7 hadi kufikia diyosisi 27 na zitaendelea kuongozeka.
Kanisa hilo limejikita katika kutoa huduma ya jamii ikiwemo huduma za afya kuanzia zahanati, sekta ya elimu katika ngazi zote, pia wana huduma ya utetezi yakupinga ukatili wa kijinsia, ulemavu wa ngozi.
Kwa miaka 60 Kanisa hilo limepita katika nyakati tofautitofauti lakini bado linaendelea kukua huku likipata ushirikiano kutoka Serikalini kwa kuzingatia ustawi wa wananchi pasipo. ubaguzi.
Taasisi za Kidini zimechangia sana maendeleo ya nchi tokea kabla ya uhuru hata baada ya uhuru.
Hospitali nyingi zimekuwa zikichangia kutoa huduma kwa wananchi na nyingine zikishirikiana na serikali katika kutoa huduma hizo.
Ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoka ushirikiano katika huduma za afya hasa pale inapowalipa watumishi mishahara kwenye hospitali ambazo zinaubia na Serikali.
Halikadhalika ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano katika kutoa huduma ya kuwatibu wagonjwa wa Kansa hasa baada ya Kanisa kutoa wazo hilo.
Ameiyomba Serikali kutilia maanani mabadiliko ya tabia nchi ili kuokoa kikazi kijacho hasa kwa kutumia njia mbadala ya mwanga wa jua.
Askofu Shoo amesema, Serikali ya awamu ya sita imeendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa sekta binafsi hasa taasisi za kidini nakuleta maendelea katika nchi.
Amewataka viongozi wa Dini na Serikali kutowaga watanzania kwa msingi wa dini au kisiasa kwani umoja na mshikamano ni msingi imara kuliko kitu chochote.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema Kanisa la KKKT wamefanyakazi kubwa sana hasa kwenye kuleta mafanikio.
Wamekuwa niwadau wakubwa hususani katika Mkoa wa Arusha kwani wanagusa wananchi katika nyanja mbalimbali hasa za Kanisa na afya,hivyo serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa kanisa hilo.
Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yamefanyika Mkoani Arusha sambamba na uwekaji jiwe la msingi katika maabara ya Sayansi ya chuo Kikuu cha Makumira.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.