Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Hemed Suleiman Abdulla amezitaka nchi za Afrika kuwa na msimamo mmoja katika kupiga vita Mapambano dhidi ya rushwa .
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwaniaba ya Rais Ally Hussein Mwinyi, Jijini Arusha.
Alisema katika kuonyesha dhamira ya dhati ya mapambano hayo Tanzania ilikuwa ni nchi ya mwanzo kusaini na kuridhia mkataba wa mapambano dhidi ya Rushwa wa mwaka 2003.
Alisema rushwa inamadhara kwa kila mmoja na kutoa rai kwa watu mbalimbali kupunguza tatizo hilo la rushwa Barani Afrika ili kuongeza kasi ya Maendeleo ya nchi mbalimbali.
Alitoa rai kwa wananchi kushiriki katika maonesho ya mabanda mbalimbali sanjari na utoaji wa taarifa za masuala ya rushwa ili kudhibiti rushwa nchini.
"Rushwa ni adui wa haki kila mmoja anawajibu wa kuikataa rushwa ikiwemo wananchi kutoa taarifa za masuala ya rushwa na naomba wakurugenzi wa Taasisi mbili za Kupambana na Rushwa kuendelea kushirikiana kwani Tanzania tumefikia hatua nzuri katika kuyashinda mapambano dhidi ya rushwa.
Ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Salum Hamduni alisema siku hiyo Maalum yanatokana na maazimio ya Mkataba wa Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa mwaka 2003 unaofikisha umri wa miaka 20 .
Alisema maadhimisho hayo yanajumuisha washiriki 700 kutoka ndani na nje ya Tanzania ambapo awali wananchi mbalimbali na viongozi walitembea matembezi ya amani ya kilomita 2 ya kupinga masuala ya Rushwa Barani Afrika.
Pia mabanda yalipo katika maadhimisho hayo yanatoa elimu mbalimbali kuhusu masuala ya rushwa na uhujumu uchumi ikiwemo kupinga matumizi ya madawa ya kulevya pia kutakuwa na kongamano la masuala ya rushwa hapo kesho ambapo Waziri Simbachawene atakuwa mgeni rasmi
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba ,Sheria,Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Haroun Ali Suleiman alishukuru ushirikiano uliopo kati ya Zanzibar na Tanzania na kusisita ushirikiano huo uendelee kudumu ili kuleta tija zaidi katika masuala ya maendeleo.
Huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene alisema Tanzania ipo tayari kushirikiana na nchi nyingine kuhakikisha mkataba wa Umoja wa Afrika wa kupambana na Rushwa unatekelezwa.
Alisema wakuu wa Nchi walichagua siku hiyo kwakujerea siku maalum ya nchi za Bara la Afrika ambapo huathimishwa kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo elimu dhidi ya rushwa kupitia vyombo vya habari,makongamano mbalimbali ili kutoa ujumbe wa masuala ya rushwa.
Alisisitiza kuwa mamlaka hizo zitapeana uzoefu na kubadilishana taarifa mbalimbali za masuala ya rushwa katika Bara la Afrika.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella aliahidi ulinzi na usalama kuimarishwa na kusisita washiriki wa mkutano huo kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Jijini Arusha .
Maadhimisho ya Siku ya Mapambano ya Rushwa Barani Afrika yaliyoanza Julai 9 -11,2023 yenye kauli mbiu ya "Mafanikio ya miaka 20 ya Umoja wa Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.