Tafiti zinaonesha ongezeko kubwa la ugonjwa wa figo, licha ya kutokana na magonjwa mengine mengi, mabukizi kwenye njia ya mkojo (UTI) na ugonjwa wa Malaria imeonekana ni sababu ya ugonjwa wa figo, hivyo, watanzania wametakiwa kujinga ili kupambana na maambukizi ya magonjwa hayo.
Akizungumza kwenye Kliniki maalum ya Matibabu ya Madakari Bingwa na wabobezi inayozndelea Mkoani Arusha, ikiwa ni siku ya pili ya kliniki hiyo, Daktari bingwa wa magonjwa ya Figo kutoka Hospitali ya Saifee Jijini Dar Es salaam Dkt. Mercy Mamunyi, ameweka wazi kuwa, magonjwa ya figo yanatokana na maambukizi kwenye njia ya mkojo pamoja na ugonjwa wa malaria na kuwaaka watanzania kuchukua tahadhari kubwa kwa magonjwa hayo.
Pia, Dkt. Mercy ameutaja ukanda wa Kaskazini kuwa ni miongoni mwa Kanda zinazoongoza kwa magonjwa ya Shinikizo la juu la damu pamoja na kisukari, Magonjwa ambayo yamekuwa sababu ya kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa ya figo kwa watu wengi.
Aidha, ameshauri Watanzania kuchukua tahadhari ya matumizi ya dawa za kienyeji kupitiliza, kutotumia dawa za hospitalini bila ushauri wa daktari, zaidi kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kujitambua na kupata matibabu ya haraka na kwa gharama nafuu na kuepukana na madhara zaidi.
Kwa mujibu wa Utafiti wa Shirika la India Nephrology, watu Milioni 84 duniani kote wanatajwa kuwa wanaugua magonjwa ya figo huku shirika la Afya duniani WHO likitaja magonjwa ya figo kuwa nafasi saba kati ya kumi kwenye kusababisha vifo vya watu wengi zaidi duniani kutokana na kutozingatiwa kwa dalili za mwanzoni za ugonjwa huo.
Ikiwa ni siku ya pili ya Kambi maalum ya Matibabu bure inayoendelea kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha, kambi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, chini ya uongozi mahiri wa Mhe.Paul Christian Makonda @baba_keagan maelfu ya wananchi wameendelea kunufaika kwa kupata huduma za vipimo, matibabu na dawa bure ikiwa ni utekelzaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt. @samia_suluhu_hassan la kusogeza huduma za aya karibu na wananchi hususani wasio na uwezo wa kumudu gharama kubwa za matibabu ya madaktari bingwa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.