Maandalizi yakielekea kwenye hatua za mwisho kwenye barabara za makutano ya Mzunguko wa Mnara wa saa (Clock Tower) kuelekea kwenye Mkesha mkubwa wa kuukaribisha mwaka 2025 unaofanyika Kimkoa Kesho Disemba 31, 2024 Jijini Arusha chini ya Uratibu na Usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda.
Sherehe hizo zinafanyika kwa mara ya kwanza Kimkoa Jijini Arusha ambapo mbali ya kusherehekea mafanikio ya mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025, imekuwa ni fursa muhimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa Mkoa wa Arusha ambao bila kulipia gharama yeyote wamekuwa wakiuza bidhaa zao na kutoa huduma kwa wananchi na wageni wanaohudhuria sherehe hizo tangu Jumamosi ya Disemba 28, 2024.
Miongoni mwa Viburudisho vitakavyokuwepo Kesho kuanzia majira ya asubuhi ni pamoja na burudani ya Muziki kutoka Dj's, Wasanii wa Bongofleva, Rhumba, Kwaya mbalimbali za Injili, Vikundi vya Kaswida, Ngoma za asili pamoja na michezo mbalimbali kwaajili ya watoto watakaokuja na wazazi na walezi wao.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.