Mabunge barani Afrika yamehimizwa kuwekeza nguvu zaidi katika kuimarisha uwekezaji wa Umma kwenye sekta ya Kilimo kujadili na kutafuta suluhu ya matatizo ya Vijana pamoja na kushirikiana na serikali zao katika kubuni na kufadhili bunifu mbalimbali za Vijana ili kuondokana na tatizo kubwa la ajira linalowakabili Vijana.
Wito huo umetolewa leo Alhamisi Oktoba 03, 2024 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, wakati alipomuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa 53 wa mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika.
Dkt. Philip Mpango amewaambia washiriki wa Mkutano huo unaofanyika Jijini Arusha kwenye Ukumbi wa Grand Melia kuwa ni muhimu Mabunge kukuza sera na programu zinazounga mkono ajira, ufadhili wa kibunifu, kutetea maboresho ya sekta ya elimu na mafunzo pamoja na matumizi ya teknolojia kwenye sekta mbalimbali kama sehemu ya kuondokana na tatizo la Ajira kwa Vijana wa Barani Afrika.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.